Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga
" Jitahidini Ubora "

Dhamira, Dira na Maadili Ya Msingi

DIRA

Kutoa Watumishi wa Afya wenye weledi ambao watatoa huduma bora za Afya katika Vituo mbalimbali vya kutolea Huduma ya Afya na kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayojitokeza.

DHAMIRA.

Chuo kilianzishwa kwa dhamira ya kutoa mafunzo ya hali ya juu ambayo yatahakikisha mwanafunzi anapata umahiri wa kukidhi mahitaji ya soko la huduma za afya katika mazingira yote.

MAADILI YA MSINGI

Maadili ya Chuo ni yale yanayohimiza uwajibikaji na uaminifu, uadilifu wa hali ya juu, elimu bora na kujali wateja.