Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga
" Jitahidini Ubora "

Karibu

Lucheri E. Kweka photo
Dkt Lucheri E. Kweka
MKUU WA CHUO

: lucheri.kweka@tangacohas.co.tz

: 255 713550106

Unakaribishwa sana katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga kinachotoa Tahasusi za Afya. Tovuti hii inaelezea mipango mbalimbali ya Taaluma za Afya, ambazo Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga inatoa, sambamba na shughuli mbalimbali zinazofanywa kama sehemu ya Dhamira na Dira ya Chuo. Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga kilianzishwa mwaka 2019 kikiwa na wanafunzi 500 baada ya kuunganisha vyuo vitatu (3) ambavyo ni Chuo ya Uuguzi Tanga, Chuo cha Madaktari wasaidizi Tanga na Chuo cha Afisa Tabibu wa Meno Tanga . Idadi ya wanafunzi imeongezeka katika Tahasusi mbalimbali za Afya. Kwa sasa Chuo kinatoa Tahasusi nne (4) za Stashahada  ya Utabibu, Uuguzi na Ukunga, Wataalamu wa Maabara na Utabibu wa kinywa na meno zote zinatolewa kwa miaka mitatu (3).
Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Tanga kina mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunza. Baada ya maelezo hayo ninatumaini yangu ya kuwa tovuti hii itakuwa ya  msaada kwako. Hata hivyo kwa chochote ambacho utashindwa kukipata tafadhali tujulishe.

 Nyote mnakaribishwa.