TAALUMA, TAFITI NA USHAURI
Dkt. Badria Kombe Mushi
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri
Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, anawakaribisha Wanafunzi, Wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga. Chuo kinatoa tahasusi za Afya zinazokidhi mahitaji ya wafanyakazi duniani kote kwa kusisitiza umahiri na ushirikishwaji. Inaeleweka vyema kwamba matatizo mengi ya kiafya na changamoto zinazoikabili dunia ya leo zinaweza kutatuliwa kwa kutoa mafunzo yenye ubora ambayo yanahakikisha mwanafunzi wanapata ujuzi wa kukidhi mahitaji ya soko kwa ajili ya huduma za afya katika mazingira yote.
Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga kina idara nne (4) ambazo ni Idara ya Utabibu, Idara ya Uuguzi na Ukunga, Idara ya Utabibu wa Meno na Idara ya Maabara ya Sayansi za Tiba.
Ofisi ya Makamu Mkuu daima iko wazi kwa wadau wanaotaka kupata taarifa mbalimbali na kuhusu mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga.
Nyote mnakaribishwa.