QUALITY ASSURANCE UNIT
Dr. Julia W. Muchunu
Head of Quality Assurance Unit
Ninayofuraha kuwakaribisha nyote kama wadau katika ukurasa wa wavuti wa Kitengo cha Uthibiti Ubora. Kitengo hiki kinafanya kazi chini ya Ofisi ya Mkuu wa Chuo kwa dhamira ya kuwezesha utendaji bora katika ufundishaji, utafiti, na huduma za jamii ili kukidhi matarajio ya washikadau wote. Dira ya Kitengo cha Uthibiti Ubora ni kuwa chombo cha Uangalizi katika masuala yote ya ubora kwa ajili ya utoaji wa tahasusi za kisasa za kitaaluma, matokeo ya utafiti, na huduma za jamii.
Tunapofanya kazi pamoja sote, ninakuhimiza uendelee kuwasiliana na Kitengo cha Uthibiti Ubora. Kitengo kitaendelea kuwa jukwaa ambapo wadau watashirikishwa katika kuhakikisha kuwa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Tanga kinaendelea kuhimiza na kuzingatia ubora katika elimu.
Nyote mnakaribishwa.